Wednesday, April 8, 2015

PESA SIO KIGEZO KWA GUARDIOLA.

MJUMBE wa bodi wa klabu ya Bayern Munich, Jan-Christian Dreesen anaamini pesa haitakuwa kigezo katika uamuzi wa Pep Guardiola juu kuongoza mkataba mwingine na mabingwa hao wa Bundesliga. Kocha huyo wa zamani wa Barcelona anatarajia kumaliza mkataba wake Juni mwaka 2016 na amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka pindi mkataba wake utakapokwisha. Bayern wanaonekana hawana haraka ya kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya ingawa mwenyekiti Karl-Heinz Rummenigge alibainisha mapema mwaka huu kuwa hakuna mazungumzo yaliyopangwa mpaka mwishoni mwa msimu. Dreesen amesema Guardiola sio aina ya kocha ambaye yuko kimaslahi zaidi akitaka kutengeneza pesa nyingi kadri awezavyo kwa angeweza kufanya hivyo sehemu nyingine wakati akijiunga na Bayern. Guardiola ameingoza Bayern kushinda mataji mawili katika msimu wake wa kwanza akiwa kocha nab ado anaweza kushinda mataji mfululizo msimu huu.

No comments:

Post a Comment