KLABU ya AS Roma imeamriwa kufunga sehemu ya uwanja wake katika mchezo wao ujao wa nyumbani baada ya mashabiki kuonyesha mabango ya kumdhalilisha mama wa shabiki wa Napoli aliyekufa kufuatia vurugu kati ya mashabiki mahasimu mwaka jana. Mashabiki hao walionyesha mabango hayo katika Uwanja wa Olimpiki wakati wa mchezo wa Serie A dhidi ya Napoli Jumamosi iliyopita. Hatua hiyo ilifikiwa na kamati ya nidhamu ya Serie A ambayo ililaani kitendo hicho na kutoa adhabu hiyo kama fundisho kwa timu zingine. Mabango hayo yalikuwa yakimlenga Antonella Leardi, mama wa shabiki wa Napoli Ciro Esposito ambaye alifariki mwaka jana ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja toka apigwe risasi wakati wa vurugu kati ya mashabiki kabla ya mchezo wa Kombe la Italia jijini Rome. Toka wakati huo Leardi amekuwa akiongoza kampeni ya kupinga masuala ya vurugu katika mechi za soka.
No comments:
Post a Comment