KIUNGO wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere amesema yuko tayari kurejea katika kikosi cha kwanza baada ya kucheza katika kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 baada ya kujiuguza kwa muda majeraha ya kifundo cha mguu. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 amefanyiwa upasuaji mara mbili katika kifundo cha mguu wake wa kushoto ambao aliumia katika mchezo dhidi ya Manchester United Novemba mwaka jana. Hata hivyo kwasasa Wilshere anaonekana kuwa fiti baada ya kucheza kwa dakika zote tisini katika mchezo huo ambao pia uliwajumuisha nyota wengine kama Mikel Arteta na Abou Diaby. Wilshere amesema unaweza kufanya mazoezi mara nyingi upendavyo lakini huwezi kuwa fiti mpaka utakapopata nafasi ya kucheza. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa anajiona yuko fiti na yuko tayari kucheza katika kikosi cha kwanza ingawa jambo hilo litaamuliwa na kocha mwenywe.
No comments:
Post a Comment