SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limeondoa vipengele vinavyodhibiti ukomo wa umri kwa wajumbe wa kamati wa utendaji. Hatua hiyo inatoa mwanya kwa rais wa CAf Issa Hayatou kuwania awamu nyingine ya uongozi wa shirikisho hilo katika uchaguzi wa mwaka 2017. Viongozi wote wa mashirikisho ya soka kutoka nchi 54 za Afrika walikubali mapendekezo hayo ambayo yaliondoa kipengele hicho. Kipengele hicho kilikuwa kinamzuia mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 70 kushikilia wadhifa wowote katika shirikisho. Hayatou mwenye umri wa miaka 68 anatarajia kuwania kiti hicho cha urais ambayo itamruhusu kuongoza hadi atakapotimu miaka 75 mwaka wa 2021.
No comments:
Post a Comment