Tuesday, April 14, 2015

RAIS WA SAMPDORIA ADAI BALOTELLI ATANG'AA AKIWA KATIKA TIMU HIYO.

RAIS wa klabu ya Sampdoria, Massimo Ferrero amedai kuwa mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli anapaswa kuchagua kwenda kujiunga na timu hiyo. Balotelli amekuwa na msimu mbaya toka atue Anfield alitokea AC Milan kwa kitita cha paundi milioni 16 majira ya kiangazi mwaka jana, akiwa amefunga mabao manne pekee katika mechi 25 alizocheza. Ferrero anaamini Balotelli mwenye umri wa miaka 24 amepoteza mapenzi yake na soka hivyo anatakiwa kwenda Sampdoria mahali ambako anaweza kurejesha kiwango chake kwasababu kutakuwa hakuna mtu wa kumfuatilia. Ferrero amesema kama Balotelli akienda Sampdoria ataweza kurejea katika kiwango chake kwani huko hakuna mtu atakayembugudhi kama atakosa bao. Rais huyo aliendelea kudai kuwa kinachomrudisha nyuma akiwa na Liverpool ni kule kukosolewa kila mara jambo ambalo linaondoa hali yake ya kujiamini hata anapopata nafasi ya za wazi kufunga.

No comments:

Post a Comment