MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amesema hana wasiwasi na kibarua chake pamoja na kikosi chake kupokea kipigo kutoka kwa Crystal Palace jana na kufifisha matumaini yao ya ubingwa. Wakiwa ugenini City walijikuta wakikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Palace na kuzusha wasiwasi wa kiwango chao baada ya kushinda mechi nne kati ya 11 walizocheza wakitofautiana na vinara Chelsea kwa alama tisa. Kipigo hicho kinaifanya City kuteleza kutoka nafasi ya pili mpaka ya nne na kuacha Arsenal wakikaa katika nafasi yao wakifuatia Manchester United katika nafasi ya tatu. Akihojiwa Pellegrini amesema kwasasa hawaifikirii Chelsea au taji la Ligi Kuu, wanachojaribu wao ni kushinda mechi zao. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 aliendelea kudai hana wasiwasi kuhusu kibarua chake kwani amekuwa akifanya kazi nzuri na anafurahia hilo.
No comments:
Post a Comment