WAKALA wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba amekiri mteja wake huyo anaweza kuondoka katika klabu ya Juventus kama akipata ofa nzuri katika majira ya kiangazi. Kiungo huyo amejiimarisha na kuja kuwa mmoja kati wachezaji bora wa soka duniani toka alipojiunga na Juventus kwa uhamisho huru akitokea Manchester United mwaka 2012. Kiwango chake hicho kimezivutia klabu mbalimbali kubwa barani Ulaya zikiwemo Paris Saint-Germain, Barcelona, Real Madrid, Chelsea na Manchester City zote zikitarajiwa kutoa ofa zao katika majira ya kiangazi. Juventus ilifanikiwa kumshawishi Pogba kusaini mkataba mpya Octoba mwaka jana ambao utamfanya kuendelea kuitumikia klabu hiyo m,paka mwaka 2019 lakini wakati wa mchezaji huyo Mino Raiola amesisitiza kuwa ni muda mchache umebakia kabla ya mteja wake hajaondoka jijini Turin. Akihojiwa wakala huyo amesema toka kuanza kwa msimu huu amepokea simu zaidi ya 2,000 kuhusu Pogba. Raiola aliendelea kudai kuwa ameshapokea ofa mbalimbali lakini hakuna hata moja iliyofikia thamani wanayohitaji na kama itapatikana hakuna shaka kuwa Pogba ataondoka Juventus.
No comments:
Post a Comment