GOLIKIPA wa Togo, Kossi Agassa amelitaka Shirikisho la Soka nchini humo kumaliza matatizo yao ya kiuongozi ili waweze kupigania nafasi ya kurejea katika michuano ya Mataifa ya Afrika. Pamoja na kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka barani Ulaya na kutinga robo fainali ya michuano hiyo mwaka 2013, Togo walishindwa kufuzu michuano ya mwaka huu iliyofanyika huko Guinea ya Ikweta. Na golikipa huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 36, ameonya kuwa nchi hiyo inahatarisha kuikosa michuano hiyo tena mwaka 2017 kutokana na matatizo yaliyopo katika uongozi wa shirikisho hilo. Agassa amesema mafanikio hayatokani na wachezaji pekee bali pia uongozi uliokuwa imara, hivyo kama mgogoro wa shirikisho lao usipokwisha ni wazi watakuja kuwa watazamaji katika michuano ijayo ya Afrika.
No comments:
Post a Comment