MENEJA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema wanatarajiwa Gareth Bale kuwepo katika mchezo wa La Liga dhidi ya Sevilla baada ya kupona majeruhi. Winga huyo wa kimataifa wa Wales, amekuwa akizumbuliwa na majeruhi hayo kwa wiki kadhaa na sasa anaweza kurejea katika mchezo unahesabika kuwa kwa mgumu kwa timu hiyo kuliko michezo yao yote minne iliyobakia msimu huu. Akihojiwa Ancelotti amesema Bale amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza na anadhani atakuwepo katika mchezo dhidi ya Sevilla. Kocha aliendelea kudai kuwa Benzema kwasasa yuko fiti kuliko baadhi ya wachezaji kwani amepumzika vyema na anaweza kuwasaidia katika mchezo huo muhimu.
No comments:
Post a Comment