BEKI wa Juventus, Giorgio Chiellini amepuuza taarifa kuwa kuna uhasama kati yake na Luis Suarez wakati watakapokutana katika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Itakuwa in mara ya kwanza kea wawili hao kukutana toka katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana wakati Suarez alipomng’ata Chiellini katika mchezo wa hatua ya makundi ambao Uruguay iliifunga Italia bao 1-0. Akihojiwa kuhusiana na hilo, Chiellini amesema atapambana na Suarez kama mshambuliaji na sio kitu kingine, kama alivyofanya kea wengine wote aliokutana nao kama Cristiano Ronaldo, Gareth bale, Karim benzema na Chicharito. Beki huyo wa kimataifa wa Italia, aliendelea kudai kuwa tukio kama lile linakufanya ukomae kea pande zote hivyo anadhani hata Suarez mwenyewe nia pekee aliyonayo in kushinda taji la lililopo mbele yao. Fainali ya michuano hiyo itakayozikutanisha Barcelona na Juvetus itapigwa katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin, Ujerumani Juni 6 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment