MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola leo amekanusha taarifa kuwa anaweza kujiunga na Manchester City msimu ujao, akidai kuwa anataka kumaliza mkataba wake na mabingwa hao wa Ujerumani. Akihojiwa na wanahabari kuelekea mchezo wao wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona utakaofanyika jijini Munich Jumatano hii, Guardiola amesema amekuwa akisisitiza mara nyingi kuwa anataka kumaliza mkataba wake. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake hivyo ni wazi kuwa msimu ujao ataendelea kuinoa Bayern. Tetesi za Guardiola kuikacha Bayern zimezuka baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na Barcelona katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa.
No comments:
Post a Comment