Thursday, May 7, 2015

LA LIGA KATIKA HATIHATI YA KUSIMAMISHWA.

LIGI Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga huenda ikasimamishwa kufuatia mgogoro baina ya bodi ya usimamizi wa ligi hiyo na serikali kuhusiana na mgawanyo wa mapato ya haki miliki ya kuonyesha mechi hizo moja kwa moja. Pande zote mbili zimeshindwa kufikia muafaka kuhusu mgawanyo huo hivyo kuna uwezekano mkubwa wa ligi hiyo kusimama ifikapo Mei 16. Kama muafaka huo ukishindwa kufikiwa kea wakati in wazi mchezo muhimu wa kuamua bingwa wa La Liga utakaowakutanisha Barcelona na Atletico Madrid unaotarajiwa kufanyika Mei 17 mwaka huu unaweza kuathiriwa. Serikali kuu imepitisha muswada mpya ambao utasimamia ugavi wa fedha zinazotokana na hati miliki ya matangazo ya mechi hizo za la Liga. Ambao unaungwa mkono na muungano wa wachezaji wa kulipwa LFP. Mkataba uliopa sasa inaziruhusu klabu mbili kubwa, Barcelona na Real Madrid kuingia mikataba yao binafsi na makampuni yanayorusha mechi zao moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment