Tuesday, May 5, 2015

LIGI YA MABINGWA AFRIKA: KWA MARA KWANZA KATIKA HISTORIA RATIBA YA MAKUNDI YAZIKUTANISHA TIMU TATU ZA NCHI MOJA.

KLABU zote tatu za Algeria zilizopo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika zimepangwa katika kundi moja kwa mara ya kwanza katika historia tukio kama hilo kujitokeza. Mabingwa watetezi wa michuano wa michuano hiyo Entente Setif itavaana na USM Alger na MC Eulma timu zote hizo zikiwa za Algeria huku Al Merreikh ya Sudan wakikamilisha timu za kundi B. Nchi 12 zenye timu zinazofanya vizuri katika michuano hiyo kwa kawaida hupata nafasi ya kutoa timu mbili lakini kutokana na Setif kuibuka mabingwa mwaka jana, Algeria waliongezewa nafasi moja katika michuano hiyo. Kundi A katika michuano hiyo litakuwa na timu za TP Mazembe ya DR Congo timu pekee iliyofuzu ambayo haizungumzi lugha ya kiarabu, Smouha ya Misri, Moghreb Tetouan ya Morocco na Al Hilal ya Sudan. Ratiba ya michuano hiyo ilipangwa katika makao makuu ya Shirikisho la Soka la Afrika-CAF yaliyopo jijini Cairo, Misri leo. Timu mbili kutoka katika makundi hayo mawili ndio zitafuzu kucheza hatua ya nusu fainali itakayokuwa na mikondo miwili Septemba na Octoba huku fainali pia ikitarajiwa kucheza kwa mikondo miwili Octoba na Novemba.

No comments:

Post a Comment