NGULI wa soka wa Brazil, Pele ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji wa kibovu cha mkojo. Pele mwenye umri wa miaka 74 alilazwa katika hospitali ya Albert Einstein jijini Sao Paulo Jumanne iliyopita ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha miezi sita. Nguli huyo ambaye amewahi kunyakuwa taji la Kombe la Dunia mara tatu akiwa na Brazil, alitibiwa maambukizi katika mkojo Novemba mwaka 2014 baada ya kuondolewa mawe katika figo. Enzi zake wakati akisakata kabumbu Pele aliichezea Brazil mechi 91 na kufunga mabao 77 huku akiteuliwa kuwa mchezaji bora wa karne na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Kwasasa nguli huyo anatumia figo moja pekee baada ya nyingine kuondolewa wakati akicheza soka.
No comments:
Post a Comment