Wednesday, May 13, 2015

SAKATA LA UHAMISHO WA NEYMAR LAIFANYA BARCELONA KUBURUZWA MAHAKAMANI.

KLABU ya Barcelona inatarajiwa kuburuzwa mahakamani baada ya jaji wa mahakama nchini Hispania Jose de la Mata kupitisha uamuzi wa kuifungulia kesi ya kukwepa kodi klabu na watu kadhaa kutokana na usajili wa Neymar. De La mata alithibitisha rais wa sasa wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu na aliyeoondoka Sandro Rosell(pichani) wote watasimamishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo wanazodaiwa kuwa walilipa fedha nyingi zaidi kea mchezaji huyo kuliko ya hesabu walizowasilisha mamlaka ya mapato. Neymar ambaye ni nahodha wa Brazil ndio mlengwa mkuu katika sakata hilo lililotokana na uhamisho kutokea Santos mwaka 2013, dili ambalo lilipelekea rais wa kipindi hicho Rosell kujiuzulu nafasi yake. Kesi hiyo inahusisha kiasi cha kodi ambacho hakikulipwa kutoka na fedha za ada walizolipwa wamiliki wa upande wa tatu wa mchezaji ikiwemo ada ya euro milioni 40 waliyolipwa kampuni ya N&N ambayo inamilikiwa na baba yake Neymar. Ada halisi ya uhamisho wa mchezaji huyo ilitajwa kuwa kiasi cha euro milioni 57.1 lakini baadae uchunguzi ulibaini kuwa uhamisho huo ulikaribia kiasi cha euro milioni 86.

No comments:

Post a Comment