SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limemfungia miaka nane ofisa mkuu wa Chama cha Soka nchini Tahiti, Reynald Temarii (pichani) kwa kwenda kinyume na maadili ya shirikisho hilo baada ya kupokea hongo ya zaidi ya euro 300,000 kutoka kwa ofisa wa zamani wa Qatar Mohamed bin Hammam. Katika taarifa yake FIFA imedai kuwa Temarii alikubalia kupokea kitita cha euro 305,640 kutoka kea Bin Hammam ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo pamoja na rais wa Shirikisho la Soka la Asia. Temarii alipokea hongo hiyo kwa ajili ya gharama za kushughulikia rufani yake aliyokata FIFA kufuatia kufungiwa kea suala linguine na kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa Temarii alipokea fedha hizo Januari mwaka 2011, kufuatia kikao chake na Bin Hammam kilichofanyika Novemba 2010 jijini Kuala Lumpur. Kutoka na kosa hilo Temarii amefungiwa miaka nane kutojishughulisha na shughuli zozote za soka kitaifa na kimataifa.
No comments:
Post a Comment