RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya, Michel Platini amesema mchezo wa soka utaingia dosari kama Sepp Blatter akichaguliwa tena kushikilia wadhifa wa urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Blatter mwenye umri wa miaka 79, anapigiwa chapuo ya kushinda uchaguzi huo kwa kipindi cha tano baada ya kudai mwaka 2011 ataachia ngazi. Akihojiwa Platini amesema kama Blatter akiendelea kuliongoza shirikisho hilo ni wazi kuwa litapoteza heshima, muonekano na mvuto wake. Platini aliendelea kudai kuwa atamuunga mkono Prince Ali Bin Al Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo unaotarajiwa mwishoni mwa mwezi huu huko Zurich, Uswisi. Platini amesema Blatter alimdanganya wakati alipodai kuwa kipindi hiki ikingekuwa cha mwisho kwake hivyo haoni sababu ya kumuunga mkono kwani kufanya hivyo ni kulirudisha soka nyuma.
No comments:
Post a Comment