KLABU ya AC Milan imethibitisha kumtimua meneja wake Filippo Inzaghi (Pichani) akiwa ametumikia nusu ya mkataba wake wa miaka miwili. Inzaghi aliyekuwa kocha wa vijana wa Milan, alichukua mikoba ya kuinoa timu ya wakubwa kiangazi mwaka jana akichukua nafasi ya Clarence Seedorf ambaye pia alitimuliwa. Baada ya msimu mbaya wa 2014-2015 ambao Milan imeshindw akufuzu michuano ya Ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya 10 katika msimamo wa Serie A klabu hiyo imeamua kuachana na kocha huyo.
Rais wa Milan, Silvio Berlusconi tayari alishaweka wazi mipango ya kutafuta kocha mpya wakiwa tayari wameshamfuata kocha wao wa zamani Carlo Ancelotti baada ya kuondoka Real Madrid. Hata hivyo, Ancelotti ameamua kupumzika kufundisha kufuatia mpango wake wa kufanyiwa upasuaji na sasa Milan tayari imeshatangaza mbadala wa Inzaghi kuwa Sinisa Mihajlovic (pichani) ambaye aliachia ngazi kuinoa Sampdoria mwishoni mwa msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment