Tuesday, June 16, 2015

KUNDI LA MASHABIKI URUSI WAJICHANGISHA KUMNG'OA CAPELLO.

KUNDI la mashabiki wa soka wa Urusi limepanga kuchangisha euro milioni 21.4 ili kununua mkataba wa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Fabio Capello. Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, mustakabali wake uko mashakani kutokana na Urusi kusuasua katika mechi za kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016. Kutokana na hilo mashabiki hao wameamua kuchangisha fedha hizo kupitia mtandao wenye kauli mbio Fabio Nenda Nyumbani. Kundi hilo lililoanzisha mtandao huo huo limedai kuwa halina uhusiano wowote na maofisa wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-RFU. Kundi hilo limefafanua kuwa linajua kuuwa RFU wakiamua kusitisha mkataba na kocha huyo watalazimika kumlipa kiasi hicho cha fedha ndio maana wameamua kujichangisha ili waweze kufanikisha hilo. Jumapili iliyopita Urusi ilichabangwa bao 1-0 na Austria na kuwaacha katika nafasi ya tatu katika kundi G hivyo kuweka matumaini yao ya kufuzu mashakani.

No comments:

Post a Comment