KLABU ya Barcelona imetangaza kuwa Dani Alves amekubalia kusaini mkataba mpya na timu hiyo leo. Alves mwenye umri wa miaka 32, alitarajiwa kuondoka baada ya mazungumzo kukwama wakati Fulani huku wakala wake akibainisha AC Milan na klabu zingine kadhaa zilionyesha nia ya kutaka huduma yake. Hata hivyo, pande zote mbili sasa zimefikia makubaliano hivyo kumaanisha ataendelea kuwepo Camp Nou mpaka majira ya kiangazi mwaka 2017. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao, klabu hiyo ilithibitisha taarifa hizo kuwa Alves amekubali kuongeza mkataba wake ambao utamaliza Juni 30, 2017. Alves amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Barcelona msimu huu ambacho kimefanikiwa kunyakuwa mataji matatu ya La Liga, Kombe la Mfalme na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil alisajiliwa kea kitita cha euro milioni 35 akitokea Sevilla mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment