Tuesday, June 9, 2015

WENGER KUMUWINDA MSHAMBULIAJI WA PORTO.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anatarajia kumuwinda mshambuliaji wa klabu ya FC Porto Jackson Martinez lakini kama atapunguza baadhi ya washambuliaji alionao. Inaarifiwa kuwa Wenger yuko tayari kuwauza Lukas Podolski, Yaya Sanogo na Joel Campbell katika kipindi hiki cha kiangazi ili aweze kukusanya fedha kwa ajili ya Martinez. Kocha huyo anataka kutoa ofa ya paundi milioni 25 kea ajili ya mshambuliaji huyo ikiwa in sehemu ya kuimarisha kikosi chake ili aweze kufukuzia taji la Ligi Kuu msimu ujao. Villarreal, Benfica na Real Sociedad wote wanamtaka Campbell wakati Sanodo yeye amepelekwa kea mkopo Crystal Palace. Kama akifanikiwa kupata fungu hilo, Martinez ndiye mshambuliaji Wenger anayemuhitaji pamoja na kuwa tayari kuna ushindani mkubwa wa nafasi hiyo kutokana na na uwepo wa Olivier Giroud, Danny Welbeck na Theo Walcott.

No comments:

Post a Comment