KLABU ya West Ham United imethibitisha kumteua Slaven Bilic kuwa kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu akichukua nafasi ya Sam Allardyce aliyetimuliwa. Bilic raia wa Croatia anarejea katika klabu ambayo amewahi kuichezea kwa miezi 18 kuanzia mwaka 1996 mpaka 1997. Akihojiwa mara baada ya uteuzi huo, Bilic amesema pamoja na changamoto atakazokabiliana nazo huko mbele lakini amefurahi kurejea tena Upton Park. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa West Ham in klabu kubwa na kuna kiti cha kipekee kwani anajiona kama yuko nyumbani hivyo anaomba ushirikiano kea viongozi, wachezaji na mashabiki ili waweze kuipeleka mbele zaidi.
No comments:
Post a Comment