TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Marekani imefanikiwa kuanza vyema kampeni zake katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kufanikiwa kuichapa Australia mabao 3-1. Mabao yaliyofungwa na Megan Rapinoe aliyefunga mawili na Christen Press yalitosha kuihakikishia timu hiyo ushindi katika mchezo huo. Marekani ambao wanashika nafasi ya pili katika orodha za ubora duniani kwa soka la wanawake, sasa wanaongoza kundi D baada ya Sweden na Nigeria kutoshana nguvu kea kufungana mabao 3-3. Kwa upande wa kundi C Japan waliitandika Switzerland bao 1-0, wakati Cameroon wao wakiirarua Ecuador mabao 6-0 na kushikilia usukani wa kundi hilo.
No comments:
Post a Comment