NGULI wa soka wa Argentina na klabu ya Boca Juniors, Diego Maradona amemkaribisha Carlos Tevez katika timu hiyo huku tetesi zikiendelea kuvuja kuwa mshambuliaji huyo wa Juventus anaweza kurejea nyumbani. Tevez mwenye umri wa miaka 31, ambaye amefunga mabao 20 katika Serie A msimu uliopita, pia amekuwa akihusishwa na tetesi na kutakiwa na klabu za Liverpool, Atletico Madrid na Paris Saint-Germain. Mshambuliaji huyo ambaye kwasasa yuko katika majukumu ya kimataifa na Argentina katika michuano ya Copa America, amewahi kuichezea Boca Juniors kuanzia mwaka 2001 mpaka 2004. Maradona aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook akimkaribisha Tevez nyumbani hivyo kuongeza uwezekano wa nyota huyo kwenda Boca. Maradona amewahi kuwa makamu wa rais wa Boca mwaka 2005 na pia amemfundisha Tevez wakati akiinoa timu ya taifa ya Argentina katika ya mwaka 2008 na 2010.
Saturday, June 20, 2015
MARADONA AMKARIBISHA TEVEZ BOCA JUNIORS.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment