TIMU ya taifa ya Serbia wametawadhwa kuwa mabingwa wapya wa michuano ya Kombe la Dunia kea vijana chini ya umri wa miaka 20 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 waliopata katika mchezo fainali dhidi ya Brazil uliofanyika jana. Bao la ushindi la Serbia liliwekwa kimiani na Nemanja Maksimovic katika dakika ya 118 baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa North Harbour uliopo huko Auckland, New Zealand. Nchi ambayo ilijimega kutoka kwa Yugoslavia mara ya mwisho kushinda taji hilo ilikuwa nchini Chile mwaka 1987. Katika mchezo mwingine wa kutafuta mshindi wa tatu Mali walifanikiwa kuwanyuka Waafrika wenzao Senegal waliocheza pungufu kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kunyakuwa nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment