Friday, June 12, 2015

NAPOLI YAPATA MBADALA WA BENITEZ.

KLABU ya Napoli imetangza kuwa Maurizio Sarri ndiye kocha atakayechukua mikoba ya Rafael Benitez aliyekwenda Real Madrid mara baada ya msimu kumalizika. Klabu hiyo ilitangaza katika mtandao wake jana kuwa Sarri ndio atakuwa kocha wa timu hiyo kea msimu wa 2015-2016 baada ya kuinoa Empoli kwa miaka mitatu. Sarri ambaye ana uzoefu mkubwa nchini Italia, msimu huu ndio ulikuwa wa kwanza kwake katika Serie A baada ya kuipandisha daraja Empoli mwaka mmoja uliopita. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 aliiongoza Empoli kumaliza katika nafasi ya 15 katika msimamo wa Serie A msimu wa 2014-2015 hivyo kumfanya kuzivutia klabu nyingi zilizokuwa zikitaka huduma yake kabla ya Napoli kumuwahi.

No comments:

Post a Comment