Friday, June 12, 2015

SIMUOGOPI MTU - BOLT.

MWANARIADHA nyota wa mbio fupi na bingwa mara mbili wa olimpiki, Usain Bolt amepuuza madai kuwa anaogopa kuchuana na Justin Gatlin wa Marekani ambaye kwsasa yuko katika kiwango cha juu. Gatlin mwenye umri wa miaka 33, amekimbia muda wa haraka zaidi kea mwaka huu katika mbio za mita 100 na 200 akitumia muda wa sekunde 9.75 na 19.68 lakini bado hajakimbia na Bolt msimu huu. Wawili hao wanatarajiwa kukutana katika mashindano ya riadha ya Dunia yanatakayofanyika jijini Beijing Agosti mwaka huu sambamba na nyota wengine kama Tyson Gay na Asafa Powell. Akihojiwa Bolt mwenye umri wa miaka 28 ambaye anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 na 200, amesema huwa anacheka watu wakimuambia kuwa anaogopa. Bolt raia wa Jamaica aliendelea kuwa amekuwa katika mchezo huo kea kipindi kirefu na hajawahi kumkwepa mtu kwani siku zote amekuwa akijitokeza na kuonyesha kuwa yeye ni bora. Bolt anatarajiwa kushiriki mbio za mita 200 zitakazofanyika jijini New York Jumapili hii.

No comments:

Post a Comment