WORLD CUP UNDER 20: MALI KUCHUANA NA UJERUMANI ROBO FAINALI.
TIMU ya taifa ya Mali sasa inatarajiwa kupambana na Ujerumani katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 itakayofanyika Jumapili hii huko Christchurch, New Zealand. Ujerumani wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuichapa Nigeria ambao in washindi wa pili wa michuano hiyo mwaka 1989 na 2005, kwa bao 1-0. Bao pekee katika mchezo huo kea upande wa Ujerumani liliwekwa kimiani na nyota wao Levin Oztunali katika dakika ya 19. Robo fainali nyingine itakayofanyika siku hiyo itawakutanisha wawakilishi wengine wa Afrika Senegal watakaokwaana na Uzbekistan huko Wellington.
No comments:
Post a Comment