Saturday, June 20, 2015

NEYMAR ATUPWA NJE COPA AMERICA.

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar anatarajiwa kuikosa michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile baada ya kufungiw akucheza mechi nne. Mshambuliaji huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 23 alionyeshwa kadi nyekundu kea kuzozana na wachezaji wa Colombia kufuatia kipigo cha bao bao 1-0 walichopata Brazil katika mchezo wao wa makundi. Nyota huyo tayari anatumikia adhabu ya kutocheza mechi moja hivyo kumfanya kutokuwepo katika mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Venezuela utakaochezwa baadae leo. Lakini Shirikisho la Soka la Amerika Kusini sasa limepitia tukio hilo na kuongeza adhabu kwa nyota huyo. Mchezaji wa Colombia Carlos Bacca ambaye pia alipewa kadi nyekundu katika tukio hilo naye amepewa adhabu ya kutocheza mechi mbili huku wachezaji wote wakipewa nafasi ya kukata rufani kama hawakuridhika na adhabu.

No comments:

Post a Comment