Saturday, June 20, 2015

DZEKO KUENDELEA KUBAKIA CITY.

WAKALA wa Edin Dzeko amedai kuwa hakuna nafasi kwa mteja wake kuondoka katika klabu ya Manchester City majira haya ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Bosnia-Herzegovina amefunga mabao sita pekee katika mechi 31 za mashindano yote alizocheza msimu uliopita na kumfanya kuhusishwa na tetesi za kuondoka City. Lakini wakala wake, Irfan Redzepagic amesisitiza hakuna ofa yeyote iliyotolewa kea mteja wake kutoka katika klabu zingine na mwenyewe anataka kuendelea kuwepo Etihad msimu ujao. Akihojiwa wakala huyo amesema kama ukisikiliza vyombo vya habari unaweza kudhani vilabu vyote vinamtaka Dzeko lakini ukweli in kwamba hakuna kitu kama hicho kwani mwenyewe bado anataka kuendelea kuitumikia City.

No comments:

Post a Comment