WAKALA wa Kevin-Prince Boateng amethibitisha kuwa kiungo huyo anaweza kujiunga tena na AC Milan katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ghana alikaa San Siro kea miaka mitatu na kufanikiwa kushinda taji la Serie A katika msimu wake wa kwanza kabla ya kuondoka kwenda Schalke ya Ujerumani Agosti mwaka 2013. Hata hivyo, Boateng anataka kuondoka Schalke baada ya kusimamishwa na klabu hiyo Mei 11 mwaka huu kufuatia kichapo walichopata dhidi ya Koln. Wakala wa Boateng, Federico Pastorello amesema kwasasa wanasubiri ofa lakini akakiri kuwa uwezekano wa kurejea Milan ni mkubwa. Milan baada ya kumtimua kocha Filippo Inzaghi na kumuajiri Sinisa Mihajlovic, wanategemewa kutenga fungu kubwa kea ajili ya usajili kiangazi hiki ili kurejesha makali yao baada ya kumaliza msimu wa Serie wakiwa nafasi ya 10.
No comments:
Post a Comment