Thursday, June 11, 2015

ROBBIE KEANE AONGEZA MKATABA GALAXY.

MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa Janhuri ya Ireland, Robbie Keane amesaini mkataba mpya na klabu ya Los Angeles Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani. Keane mwenye umri wa miaka 34, amesgafunga mabao 55 katik mechi 91 alizocheza toka amehamia Marekani mwaka 2011. Muda mkataba haukuwekwa wazi lakini kocha wa timu hiyo Bruce Arena amesema amefurahi kuona kuwa Keane ataendelea kuwa mchezaji wao kwa miaka kadhaa ijayo. Keane ataungana jijini California na mchezaji mwenzake wa zamani katika klabu ya Liverpool Steven Gerrard wakati atakapowasili Julai mwaka huu.

No comments:

Post a Comment