KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Steve McClaren ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Newcastle United akiziba nafasi ya John Caever aliyetimuliwa hivi karibuni. Kocha huyo pia ametajwa kuwepo katika bodi ya timu hiyo, huku Mike Ashley akiiacha nafasi yake katika bodi na kubaki kuwa mmiliki tu. McClaren ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu huku kukiwa na uwezekano wa kuongezwa, amesema kuwa anatambua wajibu wake ni kuwapa mashabiki na wapenzi timu ambayo watajivunia. McClaren aliiongoza Uingereza mwaka 2006 mpaka 2007, lakini pia amewahi kuzifundisha klabu za Middlesbrough, Nottingham Forest pamoja na Wolfsburg ya Ujerumani.

No comments:
Post a Comment