Thursday, June 11, 2015

ZICO ATANGAZA NIA FIFA.

HUKU kukiwa bado hali si shwari ndani ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Zico amepania kugombea ya urais wa shirikisho hilo baada ya kukiri kufadhaishwa na kashfa za ufisadi katika uongozi wa FIFA. Zico mwenye miaka 52 na ambaye jina lake halisi ni Arthur Antunes Coimbra, amesema ni wajibu wake kugombea.  Akizungumza na wanahabari katika kituo chake cha kufundisha soka kilichopo jijini Rio de Janerio, Zico amesema ni huzuni kwa wanamichezo kuona kile kinachotokea katika soka leo hii. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kutokana na uzoefu na ujuzi alionao anaona atakuwa mtu sahihi wa kulisafisha shirikisho hilo ndio maana anataka kujitosa kugombea nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment