Thursday, June 11, 2015

SAKHO ADAI HAONDOKI LIVERPOOL.

NYOTA wa Liverpool, Mamadou Sakho amekanusha tetesi za kuondoka na kuongeza kuwa bado anataka kuthibitisha ubora wake Ligi Kuu. Sakho mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Liverpool akitokea Paris Saint-Germain mwaka 2013 kea ada ya euro milioni 20.6, lakini mpaka sasa ameshindwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza akiwa ameanza katika michezo 16 katika msimu huu ambao aliandamwa na majeruhi. Pamoja na hayo, Sakho ambaye amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kitakachocheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Albania, amesema hana mpango wowote wa kutafuta klabu nyingine na anamatumaini ya kuimarisha katika kipindi kifupi kijacho. Sakho amesema msimu uliopita haukuwa mzuri sana kwake kwakuwa aliandamwa na majeruhi mengi lakini kwasasa yuko fiti anajisikia vyema kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment