Thursday, June 11, 2015

WILSHERE AKUBALI YAISHE.

KIUNGO wa Arsenal, Jack Wilshere amekubali mashitaka ya Chama cha Soka cha Uingereza-FA kea kosa la kuanzisha wimbo wa kuwaponda mahasimu wao Tottenham Hotspurs wakati wa sherehe za Kombe la FA. Wilshere alichukua kipaza sauti na kuanzisha wimbo huo huku mashabiki wa Arsenal waliojitokeza kulilaki kombe hilo nao wakiitikia kea sauti. Pamoja na kuwepo katika makujukumu ya kimataifa Wilshere alipelekewa mashitaka hayo na kuyakubali huku akikiri kushangazwa nayo. Wilshere mwenye umri wa miaka 23 ambaye aliomba radhi katika ukurasa wake mtandao wa kijamii wa twitter mara baada ya tukio hilo anatajiwa kuwepo katika kikosi cha Uingereza kinachokwaana na Slovenia Jumapili hii.

No comments:

Post a Comment