KOCHA wa timu ya taifa ya Chile, Jorge Sampaoli amekiri kuwa pamoja na magumu waliyokuwa nayo katika mchezo wao ufunguzi wa kundi A wa michuano ya Copa America dhidi ya Ecuador lakini anadhani walistahili ushindi wa mabao 2-0 waliopata. Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Arturo Vidal na Eduardo Vargas yaliisaidia Chile kupata ushindi huo muhimu ingawa Sampaoli anadhani bado wanahitaji kuimarika zaidi kama wanataka kushinda taji la michuano hiyo. Akihojiwa Sampaoli amesema waliweka mipango yao kama walivyofanya katika mchezo dhidi ya Brazil, ambapo ilikwenda vyema katika kipindi cha kwanza lakini walihangaika kipindi cha pili baada ya kushindwa kufunga. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Ecuador waliwapa wakati mgumu kwani na wao walikuwa wakishambulia kwa kasi hivyo in wazi wanapaswa kujiandaa zaidi kea ajili ya mechi zao zijazo ili waweze kufika mbali. Chile itakwaana na Mexico Juni 15 katika mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya michuano hiyo.

No comments:
Post a Comment