MICHUANO ya Kombe la Dunia la wanawake inayoendelea huko Canada imeendelea tena huku sare zikitawala katika michezo ya jana. Mabingwa wa Ulaya Ujerumani wao waling’ang’aniwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Norway huku wenyeji Canada wao wakishindwa kutambiana na New Zealand kwa kwenda sare ya bila kufungana. Canada wameendelea kuongoza kundi A wakiwa na alama nne katika michezo miwili waliyocheza wakifuatiwa na China na Uholanzi ambao wote wana alama tatu huku New Zealand wakiburuza mkia kwa kuwa na alama moja. Kwa upande wa kundi B Ujerumani na Norway wameendelea kuongoza wote wakiwa na alama nne wakifuatiwa na Thailand waliopo nafasi tatu kea kuwa na alama tatu na Ivory Coast wanaburuza mkia akiwa hawana alama yeyote. Michuano hiyo inaendelea tena leo ambapo katika kundi C mabingwa watetezi Japan watavaana na Cameroon huku Switzerland wao wakiivaa Ecuador na kundi D Marekani watacheza na Sweden huku Australia wakiwavaa mabingwa wa Afrika Nigeria.

No comments:
Post a Comment