Friday, June 12, 2015

XAVI ATAMBA KUCHUKUA MAKOMBE ZAIDI AKIWA NA AL-SADD.

KIUNGO mpya wa klabu ya Al-Sadd ya Qatar, Xavi amesisitiza amejiunga na timu hiyo kwa lengo la kushinda mataji zaidi na kuchangia ujuzi na uzoefu wake kwa lengo la kukuza hadhi ya soka nchini humo. Kiungo huyo mkongwe aliitumikia Barcelona katika mchezo wa mwisho Jumamosi iliyopita wakati alipocheza katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuitandika Juventus kwa mabao 3-1. Xavi alikuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Barcelona lakini badala yake alikubali kuhamia Qatar na alitambulishwa rasmi jana mbele ya wanahabari. Akihojiwa Xavi amesema anajisikia furaha kuwepo hapo na bado ana hamu ya kushinda mataji kama alivyokuwa akichipukia. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania aliendelea kudai kuwa anataka kushinda taji la ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa bara la Asia huku wakati huohuo akitumia uzoefu wake kusaidia kuinua soka la nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment