Tuesday, June 16, 2015

WORLD CUP UNDER 20: SENEGAL KUKWAANA NA BRAZIL KATIKA NUSU FAINALI KESHO.

GOLIKIPA wa Senegal, Ibrahima Sy anauhakika wa kuendelea na ushujaa wake wa kuokoa mikwaju ya penati kama atahitajika kufanya hivyo katika mchezo wao wa nusu fainali wa michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 dhidi ya Brazil kesho. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 amekuwa kipnezi cha mashabiki mapema katika michuano hiyo kutokana na umahiri wake anapokuwa langoni. Umaarufu wake ulizidi wakati alipookoa michomo mitatu ya penati katika mchezo dhidi ya Ukraine katika hatua ya timu 16 bora. Akihojiwa Sy amesema ana kipaji cha kuokoa mikwaju ya penati, hawezi kuelezea in kea namna gani anaweza kufanikisha hilo kwani ni kitu ambacho anacho. Mshindi katika mchezo huo atakwaana na aidha Serbia au Mali katika mchezo wa fainali w michuano hiyo utakaofanyika huko Auckland, New Zealand Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment