KLABU ya Bayern Munich imekubaliana kiwango cha ada na Juventus kwa ajili ya kiungo Arturo Vidal. Nyota huyo wa kimataifa wa Chile anatarajia kuhamia kwa mabingwa hao wa Bundesliga kwa kitita cha euro milioni 40 baada ya wakala wake Fernando Felicevich kukutana na klabu hiyo kuzungumzia maslahi atakayopata katika mkataba wa miaka mitano atakaopewa. Meneja wa Bayern, Pep Guardiola amekuwa akimuwinda kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kutakiwa na klabu za Real Madrid na Arsenal katika kipindi hiki cha kiangazi. Mkataba wa Vidal katika klabu ya Juventus unamalizika majira ya kiangazi mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment