KIUNGO mpya wa klabu ya Manchester United, Morgan Schneiderlin amesema kushuka daraja na Southampton lilikuwa jambo zuri kuwahi kumtokea katika maisha yake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na United kwa kitita cha paundi milioni 25 baada ya kuitumikia Southampton kwa kipindi cha miaka saba. Schneiderlin ana uhakika anaweza kuisaidia United kumaliza ukata wao wa miaka miwili bila taji kwani sasa anataka kushinda kila kitu. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesema wakati aliposhuka daraja na Southampton mwaka 2009 lilikuwa jambo lililomsaidia kwa kiasi kikubwa kwa aliimarisha mchezo wake mpaka kufikia alipo sasa. Mara ya mwisho United kupata taji ilikuwa mwka 2013 waliponyakuwa taji la Ligi Kuu na Schneiderlin anadhani wakati wa kurejesha furaha kwa mashabiki umefika.
No comments:
Post a Comment