Thursday, July 16, 2015

LEVERKUSEN YAMNASA TAH KUTOKA HAMBURG.

KLABU ya Bayer Leverkusen imefanikiwa kumsajili beki wa Hamburg Jonathan Tah kwa kitita cha euro milioni 10. Leverkusen ilithibitisha kumsajili mapema leo, huku nyota huyo ambaye ni nahodha wa timu ya Ujerumani kwa vijana chini ya umri wa miaka akipewa mkataba unaomalizika Juni mwaka 2020. Mchezaji huyo anakuwa wa tatu kusajiliwa na Leverkusen kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya kuwa tayari wameshazinasa saini za mshambuliaji wa zamani wa Freiburg Admir Mehmedi na Kyriakos Papadopoulos kutoka Schlake. Akihojiwa Tah amesema amafurahi kumalisha usajili huo na ana matumaini ya kuimarika katika timu hiyo.

No comments:

Post a Comment