Monday, July 6, 2015

BARCELONA YAMNASA TURAN KUTOKA ATLETICO.

KLABU ya Barcelona, imemsajili kiungo wa kimataifa wa Uturuki, Arda Turan kutoka Atletico Madrid kwa kitita cha paundi milioni 24. Katika taarifa yake klabu hiyo imedai kuwa ada hiyo inaweza kuongezeka mpaka paundi milioni 29. Turan mwenye umri wa miaka 28, hataweza kuichezea Barcelona mpaka Januari mwakani kutokana na adhabu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA waliyopewa ya kutosajili mpaka 2016. Nyota huyo amefunga mabao 22 na kutengeneza mengine 32 katika msimu minne ambayo amekuwa Atletico toka ajiunge nao akitokea Galatasaray mwka 2011. Barcelona wamefungiwa kusajili wachezaji mwaka huu baada ya kukutwa na hatia ya kufanya usajili wa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 18 kinyume na sheria za FIFA.

No comments:

Post a Comment