Thursday, July 23, 2015

BAYERN YATHIBITISHA ARTURO VIDAL ALMOST A DONE DEAL.

KLABU ya Bayern Munich, imethibitisha kuwa kiungo Arturo Vidal atajiunga na timu hiyo akitokea Juventus kwani sasa kilichobakia ni kufanyiwa vipimo vya afya na kusaini mkataba wake. Mabingwa hao wa Ujerumani walikubali kutoa ada ya euro milioni 40 iliyotakiwa na Juventus kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Chile, Alhamisi iliyopita. Baadae ofisa mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alifafanua kuwa uhamisho huo unatarajiwa kukamilika baada ya vilabu vyote na mchezaji kukubaliana masuala ya fedha. Lakini taarifa zilizotoka leo zimedai kuwa kwasasa kila kitu kiko sawa na Vidal mwenyewe ameshafikia makubaliano binafsi ya mambo ya kifedha na kilichobakia sasa na vipimo vya afya na kusaini mkataba wenyewe. Vidal anayecheza nafasi ya kiungo wa kati anachukuliwa na wengi kama mbadala wa Bastian Schweinsteiger ambaye aliondoka Allianz Arena na kwenda Manchester United mapema mwezi huu.

No comments:

Post a Comment