Thursday, July 23, 2015

BARCELONA YAKANUSHA KUPOKEA OFA KWA AJILI YA PEDRO.

RAIS wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amekanusha klabu hiyo kupokea ofa yeyote kwa ajili ya Pedro ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Ligi Kuu ya Uingereza kipindi hiki cha kiangazi. Chelsea, Manchester United na Arsenal zote zinaaminika kumuwinda nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 27. Kiungo wa Barcelona Sergio Busquets amekiri mchezaji mwenzake huyo katika klabu na timu ya taifa ana mashaka ya kubakia katika timu hiyo kutokana na kutokuwa na uhakika na nafasi yake katika kikosi cha kwanza. Hata hivyo, Bartomeu ambaye amechaguliwa tena mwishoni mwa wikiendi iliyopita kuingoza Barcelona kwa kipind cha miaka sita ijayo, amesema klabu haijapokea ofa kwa ajili ya mchezaji yeyote mpaka sasa. Bartomeu aliendelea kudai kuwa meneja wa klabu Luis Enrique alishweka wazi kuwa timu yeyote inayohitaji mchezaji kutoka Barcelona ni lazima wafikie dau lililowekwa katika mikataba yao.

No comments:

Post a Comment