Thursday, July 23, 2015

BENITEZ ASISITIZA RAMOS HANG'OKI NG'O.

MENEJA mpya wa Real Madrid, Rafael Benitez amesema beki Sergio Ramos ana asilimia 100 za kubakia katika klabu hiyo kufuatia tetesi kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania anaweza kwenda Manchester United. Meneja wa United, Louis van Gaal alidokeza mapema wiki hii kuwa anaweza kumuwania Ramos mwenye umri wa miaka 29 ambaye amebakisha miaka miwili katika mkataba wake Madrid lakini anaweza kukwamishwa na kiwango chake cha mshahara. Pia baadae zikazuka tetesi zingine kuwa Ramos anaweza kujiunga na United kama sehemu ya mpango wa kubadilishana na golikipa David De Gea mwenye umri wa miaka 24. Hatahivyo, Benitez akizungumza na wanahabari mapema leo huko Melbourne, Australia amesema De Gea sio mchezaji wao na Ramos ni nahodha wao na mchezaji muhimu kwao. Benitez amesema anataka Ramos abakie hapo na iko wazi kwake na kwa klabu kuwa atendelea kuwepo hapo msimu ujao. Madrid wanajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Manchester City unaotarajiwa kuchezwa kesho ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya timu hizo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi zao.

No comments:

Post a Comment