RAIS wa Shirikisho la Soka la Duniani-FIFA, Sepp Blatter amesema ana dhamira ya safi na yeyote anayemuita fisadi anapaswa kushitakiwa na kwenda jela. Blatter mwenye umri wa miaka 79 alitangaza mwezi uliopita kuwa anatarajia kuachia ngazi wadhifa wake huo kufuatia uchunguzi wa kashfa ya ufisadi unaoendelea katika shirikisho hilo. Akihojiwa na gazeti moja la Ujerumani, Blatter amesema hajafanya lolote baya na atakwenda peponi pindi uhai wake utakapofikia kikomo. Blatter amesema yeyote anayemuita yeye fisadi kwasababu ya tuhuma zinazolikabili shirikisho hilo anadhani anapaswa kwenda jela kwakuwa yeye ni msafi.
No comments:
Post a Comment