Friday, July 10, 2015

GERRARD AMTOLEA UVIVU STERLING.

NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Liverpool, Steven Gerrard amemwambia Raheem Sterling kufanya maamuzi kama anataka kuondoka katika timu hiyo baada ya kukosa siku mbili za mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao. Winga huyo ambaye hataki kujumuishwa katika kikosi kitakachoanza ziara nchini Australia na Asia, anawindwa na Manchester City baada ya kumwambia meneja wa Liverpool Brendan Rodgers nia yake ya kuondoka. Liverpool walianza maandalizi yao ya msimu mpya juzi bila Sterling ambayo aliiarifu klabu kuwa hataweza kuhudhuria kutokana na kuumwa na kutoa madai hayo pia jana. Akihojiwa Gerrard amesema hafurahishwi na hali hiyo kwani haoni kama kuna umuhimu na kinachotakiwa kufanywa ni wote kuchukua maamuzi magumu. Gerrard aliendelea kudai kuwa Sterling anapaswa yeye mwenyewe kumfuata mmiliki na Rodgers na kuzungumza nao kile anachohitaji na sio kutoa visingizio ambavyo havina maana.

No comments:

Post a Comment