Saturday, July 4, 2015

KOMBE LA DUNIA WANAWAKE: BASSETT AENDELEA KUWEWESEKA BAADA YA KUINYIMA UINGEREZA NAFASI YA KUCHEZA FAINALI.

BEKI wa kimataifa wa Uingereza, Laura Bassett amesema amevunjika moyo kwa kujifunga bao dakika za majeruhi ambalo lilizima ndoto za timu ya taifa ya nchi hiyo ya wanawake kushinda taji la Kombe la Dunia huko Canada. Uingereza ilichapwa mabao 2-1 na Japan katika mchezo nusu fainali baada ya Bassett mwenye umri wa miaka 31 kujifunga zikiwa zimebaki sekunde chache muda wa kawaida kumalizika. Akihojiwa Bassett amesema mara baada ya kujifunga hakuweza kupumua vyema na alikuwa akitaka ardhi ipasuke na kummeza. Tukio hilo limemfanya mwanadada huyo kushindwa hata kuzungumza na wazazi wake toka wakati huo. Lakini kocha wa Uingereza Mark Sampson ambaye amemfananisha Bassett na shujaa, amesema anatarajia kumtumia katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Ujerumani utakaofanyika baadae leo huko Edmonton.

No comments:

Post a Comment